Meneja wa Habari na Mawasilino wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Ahmed Ally amezitaka klabu za Young Africans na Azam FC kupambana na kuweka misingi itakayoziwezesha kufika mbali kwenye Michuano ya Kimataifa.

Simba SC imesalia kwenye Michuano ya Kimataifa Msimu huu 2021/22, ikishiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika, huku Azam FC na Young Africans zikitolewa mapema.

Ahmed amewasilisha ujumbe huo kwenye klabu hizo ambazo ni mshindani wa kweli wa Simba SC kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu, kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Licha ya ujumbe huo kuandikwa kwa njia ya utani, lakini una maana kubwa kwa kuzikumbusha Young Africans na Azam FC kupambana ili kufika ilipo Simba SC kwa sasa.

Ahmed ameandika: Kwenye Long Distance Hamasa tulipita Azam Complex tukacheza sana pale getini kwao
Meneja wa Uwanja Bi Sikitu Kilakala alitupokea na akafurahia ujio wetu

Tulipita Azam Complex kuwakumbusha Azam Fc kuwa mmefanikiwa kutengeneza miundo mbinu bora ya soka sasa tengenezeni timu, hakuna Kombe la Miundombinu

Natamani siku moja WASEMAJI watatu tunakua busy na CAF sio kama sasa hivi niko peke yangu nakua kama nawaonea hivi @zakazakazi

@hbumbuli halafu wananionea sana wivu??

Maendeleo mazuri ni maendeleo ya wengi, Wengi tukiwa na maendeleo kila mtu atakua busy na mambo yake
Wenye maendeleo ya kimpira hapa Tanzania ni sisi peke yetu matokeo yake wengine wamekalia kupokea wageni kwa sababu hawana cha kufanya, imagine wangekua na mechi ya robo fainali wangefanya hivyo ???

Tukifanikiwa kutinga Nusu Fainali tutapita na Jangwani tutaimba na kucheza kisha tuwakumbushe historia wanayojivunia haitowasaidia popote.

SIMULIZI: “Sitarudia tena ukahaba, kilichonipata huko siwezi kusahau!”
Francis Baraza: Tunataka kwenda kimataifa 2022/23