Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) Shally Raymond amewataka Wabunge wanawake kuwahamasisha wanawake nchini kushiriki katika uchumi wa madini ili waweze kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Ameyasema hayo Aprili 23, 2022 wakati akifungua Semina kwa Wabunge Wanawake Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Msekwa bungeni Dodoma iliyolenga kuwajengea uwezo wabunge hao kutambua fursa zilizopo katika Sekta ya Madini, kujua namna shughuli za sekta zinavyofanyika na hatimaye kuwa sehemu ya wahamasishaji na kushiriki katika uchumi huo.
Ameongeza kuwa, semina hiyo itawasaidia wabunge hao kuitazama Sekta ya Madini kwa jicho la tofauti na kuwataka kuifikisha elimu waliyoipata katika ngazi zote kuanzia kwenye familia, jamii na maeneo wanayowawakilisha wananchi.
‘’ Wanawake ni viungo muhimu katika serikali na jamii, naomba tutumie elimu hii kuwaelimisha wananake kushiriki katika uchumi wa madini ili kuepukana na tatizo la ukosefu wa ajira na kujipatia vipato,’’ amesema Shally.
Aidha, ametumia fursa hiyo kuipongeza wizara ya Madini kutokana na kuendelea kuimarika kwa mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa hadi kufikia wastani wa asilimia 7.3 kutoka wastani wa asilimia 6.5 kwa kipindi cha mwaka 2020.
Naye, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema wizara imeona umuhimu wa kuujengea uelewa umoja huo ili kutoa hamasa kwa wanawake kushiriki katika uchumi wa madini baada ya kuona kuwa shughuli nyingi katika Sekta ya Madini bado zinafanywa na wanaume.
Amesema kutokana na tofauti hiyo, Serikali kupitia wizara ya madini inaendelea kuchukua hatua ili wanawake wengi waweze kushirikki katika shughuli hizo na kuongeza kuwa, tayari Rais Samia Suluhu ameweka mazingira ya kuwawezesha wana
Semina hiyo imeratibiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).