Kisa kipya cha ugonjwa wa Ebola kimethibitishwa kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba ya Kijamii ilisema katika taarifa iliyotolewa April 22, 2022.

Mwanaume mwenye umri wa miaka 31 alifariki kutokana na ugonjwa huo katika mji wa Mbandaka, mji mkuu wa jimbo la Equateur nchini DRC, taasisi hiyo ilisema.

Mgonjwa alianza kuonyesha dalili mnamo Aprili 5, lakini hakutafuta matibabu kwa zaidi ya wiki moja.

Alilazwa katika kituo cha matibabu ya Ebola Aprili 21, 2022 na alifariki baadaye siku hiyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema katika taarifa yake.

Mlipuko wa awali wa Ebola nchini ulitangazwa zaidi ya miezi minne iliyopita, mnamo Desemba 2021.

Waziri wa Mifugo amsimamisha kazi mkandarasi
Njaa yasababisha mama amzike mwanae usiku wa manane