Mwili wa Rais Emilio Mwai Kibaki umewasili katika majengo ya Bunge nchini Kenya kwa ajili ya kuagwa na viongozi wa ngazi ya serikali.
Leo hii mwili huo utaagwa na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Rais William Ruto, mawaziri, mabalozi, wakuu wa jeshi na viongozi wengine wakuu wa serikali.
Kesho Jumanne na Jumatano itakuwa zamu ya wananchi wa kawaida kuuaga mwili wa Hayati Kibaki ndani ya majengo ya bunge la taifa.
Misa ya kitaifa ya kumuaga Hayati Kibaki itafanywa siku ya Ijumaa tarehe 29, halafu rais huyo watatu wa Kenya atazikwa Jumamosi Aprili 30 nyumbani kwake huko Othaya Nyeri.