Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameitabiria makubwa klabu ya Simba SC, baada ya kushindwa kufikia lengo la kutinga Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2021/22.

Simba SC ilitolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo Jumapili (April 24), kwa changamoto ya mikwaju ya Penati 4-3, baada ya timu hizo kushinda 1-0, kila mmoja akishinda kwake.

Rais Samia ambaye bado yupo ziarani Nchini Marekani amesema: “Sijawahi kupata kulifurahia zaidi soka la Tanzania zaidi ya mara mbili kwa mwaka furaha yangu ya kulifurahia soka la Tanzania ni mara moja tu kwa mwaka ni pale tu klabu ya Simba SC inapotinga hatua za robo fainali za Africa CAF hakika Simba SC ni wakuigwa na klabu za Tanzania”

“Nahakika uko mwaka watarejea na kombe. kujaribu au kuuliza sio ujinga ni kutaka kujua zaidi hivyo Simba Sc wanavyofika kila msimu robo upo msimu wataibuka na ubingwa”

Mafanikio ya Simba SC kutinga Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika, yametetea nafasi ya Tanzania kupeleka timu nne kwenye Michuano ya Shirikisho Barani Afrika ‘CAF’ upande wa vilabu msimu ujao wa 2022/23.

Hii itakua mara ya tatu kwa Tanzania kupeleka timu nne kwenye michuano hiyo, ambapo mara ya kwanza ilikua msimu wa 2019/20 kisha 2021/22, na mara zote Simba SC imekua ikisababisha hilo kwa mafanikio ya kufika Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Msimu wa 2018/19 Simba SC ilifika Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na kutolewa na TP Mazembe ya DR Congo kwa kufungwa 4-1, na msimu wa 2020/21 ilitolewa katika hatua hiyo na Kaizer Chief ya Afrika Kusini kwa kupoteza mabao 4-3.

Haji Manara akubali uwezo wa Henock Inonga
Pablo: Tusahau yaliyopita, tuikabili Young Africans