Maafisa wa usalama wanaoshughulikia kesi ya rapa A$AP Rocky wametoa taarifa ya kupatikana kwa kipande cha video kinachoonesha sehemu ya shambulio alilolifanya rapa huyo mwezi Novemba mwaka jana na kusabisha majeraha kwa mmoja wa watu waliokuwapo katika eneo husika.
Polisi wa Los angeles wamesema kuwa licha ya kupatikana kwa video hiyo, bado kuna utata juu ya bunduki iliyoonekana kwa kuwa haifanani na bunduki kadhaa zilizokutwa nyumbani kwa rapa huyo baada ya upekuzi uliofanywa mapema wiki iliyopita.
Polisi hao wamesema kuwa bunduki zilizopatikana nyumbani kwa Rocky hazikuwa zile zilizotumika kufyatua risasi kwa sababu ukubwa wa bunduki hizo haukulingana na maganda ya risasi yaliyopatikana kwenye eneo la tukio.
Pamoja na kutoa taarifa hiyo, Polisi wameweka bayana kuwa baada ya uchunguzi wa kina wamegundua kuwa bunduki zote zilizokutwa katika nyumba ya A$AP Rocky zilipatika kihalali hivyo kwa upande huo shaka juu ya umiliki wa silaha hizo imeondoka huku umakini ukielekezwa zaidi kwenye kutafuta bunduki iliyotumika katika shambulio hilo.
Asap Rocky ambaye jina lake halisi na Rakim Mayers anadaiwa kuwa alikwenda nyumbani kwa mwanaume anayefahamiana naye mtaani usiku wa Novemba 6, 2021, kabla ya kudaiwa kumpiga risasi kadhaa wakati washambulio analoshutumiwa nalo rapa huyo.
Kwa mujibu wa kanuni ya adhabu za makosa ya jinai ya Calfornia juu ya kesi inayomkabili Rocky, endapo atakutwa na hatia, rapa huyo anaweza kufungwa jela kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja na faini ya hadi$1,000 ambazo ni zaidi ya Milioni 2.3 za Tanzania.