Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameipongeza Kampuni ya Azam Media kwa kuwa mstari wa mbele, kuhakikisha Soka la Tanzania na michezo mingine inakua kwa kasi.

Rais Samia ametoa pongezi hizo alipozungumza na Azam TV, leo Jumatano (Mei 04) Ikulu Dodoma, ambapo amesema kampuini hiyo imejitahidi kuwekeza kwa dhati katika michezo.

Amesema anaushukuru Uongozi wa kampuni hiyo kwa kuwekeza katika tasnia ya michezo hasa mchezo wa Soka, kupitia Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo imeendelea kuwa maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.

“Ninawashukuru sana kwa kazi kubwa mnayoifanya, katika michezo mmefanya kitu kikubwa sana, huku kwenye mipira mmewekeza na ninaona juhudi zenu.”

“Mmetoa udhamini kwenye hivyo vuilabu vya mpira, nimewasilia wanawashukuru, kwa hiyo na mimi niwashukuru kwa niaba yao pia, kwa hiyo mnafanya kazi nzuri, hongereni” amesema Rais Samia alipohojiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando

Azam Media kwa zaidi ya misimu minne imekua ikidhamini Ligi Kuu upande wa Matangazo ya TV, na msimu huu kwa mara ya kwanza itatoa zawadi ya Bingwa shilingi milioni 500, huku timu nyingine shiriki zikitarajia kupata zawadi kwa nafasi watakazoshika kwenye msimamo, baada ya Ligi kufikia ukingoni mapema mwezi Juni.

Drake aendelea kuweka rekodi ya mikataba minono
Watu wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa