Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha imemuachia huru aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 jela kwa unyangányi wa kutumia silaha.

Jaji aliyesikiliza rufaa hiyo, Ezedekia Kisanya amesema kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ikiwemo kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili.

Jaji amesema watakuwa huru endapo watakuwa hawana kesi nyingine kwenye Mahakama yoyote.

Februari 14, 2022 Mahakama hiyo ilianza kusikiliza hoja 14 za waleta rufani kupinga adhabu ya hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha

Ole Sabaya anabaki akikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi, ambapo inadaiwa Sabaya na wenzake walichukua rushwa ya Tsh. Milioni 90 kutoka kwa Mfanyabiashara Mroso.

Biden amteua Karine Jean-Pierre kuwa msemaji mkuu wa Serikali
Henock Inonga akabidhiwa Tuzo, Ahmed Ally ashtukizwa