Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kesho itakuwa nyumbani ikimkaribisha Mtibwa Sugar katika Dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara utakaopigwa saa nane kamili mchana (14:00).
KMC chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana imefanya maandalizi yake ya mwisho leo ya kuwakabili Mtibwa Sugar ya Turiani Mkoani Morogoro na kwamba kikosi kiko tayari kwa mtanange huo.
Katika mchezo huo ambao KMC ni mwenyeji Kocha Mkuu Hitimana amekuwa na wakati mzuri wakufanya maandalizi na kwamba licha ya kuwa mchezo utakuwa na ushindani mkubwa lakini kama Timu imejidhatiti kupata alama tatu muhimu.
“Tunakwenda kucheza na Mtibwa Sugar ,tunafahamu kuwa ni Timu nzuri na imekuwa na wakati mzuri kwenye michezo yake hivi karibuni, lakini KMC inawachezaji wazuri na bora ambao sikuzote wamekuwa tayari kuipambania Manispaa ya Kinondoni ipate matokeomazuri hivyo mashabiki msiwe na wasiwasi Timu ipo imara kwenye mchezo huo.”
“Michezo yetu hivi karibuni hatujapata matokeo rafiki,lakini tunawaahidi mashabiki zetu kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja na kwa kuanza tunakwenda kupambana uwanjani katika mchezo wa kesho, hivyo kikubwa wazidi kuwasapoti wachezaji kwakuja uwanjani.
KMC hadi sasa imecheza michezo 22 ya ligi Kuu ya NBC na kukusanya jumla ya alama 24, nakuwa kwenye nafasi ya 11 na kwmaba mchezo wa kesho inahitaji ushindi ili kujitoa kwenye nafasi hiyo na kupanda katika nafasi za juu, jukumu kubwa kwa mashabiki ni kuzidi kuwasapoti kwa namna yoyote pale inapokuwa uwanjani.
Imetolewa leo Mei 11
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC