Naibu rais William Ruto hatimaye amemtangaza mgombea mwenza wa muungano wa Kenya Kwanza ambaye ni Rigathi Gachagua kwenye wadhifa huo muhimu katika safari yake ya kutafuta kura za kuingia Ikulu.
Eneo la Mt Kenya limetajwa kuwa muhimu pakubwa kwa wagombea wa urais kutokana na wingi wa kura
Chaguo la mgombea mwenza ndani ya Kenya Kwanza na Azimio la Umoja limekuwa likitajwa kuwa kadi inayoweza kusaidia au kuzamisha miungano hiyo.
Imekuwa afueni kwa wanahabari ambao wamekuwa wakipiga kambi mtaani Karen tangu Jumamosi Mei 14 walipokuwa wameahidiwa tangazo hilo litatolewa.
Hata hivyo, mambo yaliharibika wakati tofauti ziliibuka kati ya wabunge waliokuwa wakimuunga mkono Gachagua na wale wa Kindiki Kithure.
Majaliwa: Watanzania tuitangaze filamu ya Royal Tour
Wakati huo huo DP Ruto alitangaza vikosi ambavyo vitakuwa vikiongozwa kampeni zake katika kila eneo kuta ni aliyekuwa gavana wa Kiambu William Kabogo, Mbunge Kimani Ichung’wa, Gavana wa Nyeri Kagwe Mutahi wataongoza kampeni za Mlima Kenya.
Wakati Naibu Ruto akitangaza mgombea mwenza, bado Wakenya wanasubiri kwa hamu kumsikia Raila akitangaza Mgombea mwenza wa Muungano wa Azimio ambapo ametoa taarifa kuwa siku ya Jumatatu antakuweka hadharani.
Katika Kura za mchujo wa Mgombea Mwenza wa Raila, Watatu walitajwa kuwa kiongozi wa Narc-Kenya Martha Karua aliyeshika namba moja, aliyekuwa mbunge wa Gatanga Peter Kenneth na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, kwa utaratibu huo.
Mpangilio huo unamaanisha Karua alipata alama za juu zaidi kati ya wenzake wagombeaji wengine kwenye mchujo huo ambapo unaonekana kumpendelea zaidi kumpa nafasi ya kuwa naibu wa Raila katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Agosti 9, 2022