Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema Uchaguzi mkuu ujao wa 2025 unaonyesha Rais Samia Suluhu Hassan atashinda kwa kishindo kutokana na Umahiri wa kazi zinazofanywa na Serikali anayoiongoza.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Uwanja wa CCM Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora wakati wa ziara ya Mheshimiwa Raishii Leo, Profesa Lipumba amemshauri Rais Samia kuendeleza kasi na umakini alionao ili ifikapo kipindi hicho aweze kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo ya MO IBRAHIM inayotolewa kwa mmoja wa Viongozi wa mataifa ya Afrika kutokana na Umahiri wake wa Uongozi.

Siku kadhaa zilizopita Profesa Lipumba alionana na Rais Samia alipomtembela Ikulu na mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha demokrasia na kasi ya maendeleo.

Kauli ya Profesa Ibrahim Lipumba, mmoja wa Viongozi wakongwe wa Upinzani inakuja kipindi ikiwa ni takribani mwaka mmoja na miezi miwili tangu kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, na hivyo kudhihirisha Uongozi unaozingatia makundi mbalimbali ya Jamii yakiwemo ya Wakulima, Wafanyakazi, Wajasiriamali na Wafanyabiashara.

Majaliwa:Migogoro mikubwa ya ardhi inashughulikiwa na timu ya mawaziri nane
Kocha Baraza ataja udhaifu wa Henock Inonga Baka