Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kuwa Serikali imeendelea kuboresha kanzidata ya usajili wa laini za simu na hadi kufikia April 30 mwaka huu asilimia 100 ya laini zinazotumika zimesajiliwa kwa alama za vidole.
Amesema hayo wakati akiwasilisa Akiwasilisha bajeti ya wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 bungeni jijini Dodoma
“Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeendelea kuendesha na kuboresha kanzidata ya usajili wa laini za simu kwa njia ya kibiometria na hadi kufikia April 30,2022 laini zote za simu 55,365,239 zimesajiliwa kwa alama za vidole sawa na asilimia 100 ya laini zote zinazotumika”
“Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeendelea kukabiliana na changamoto za ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hapa nchini, Mamlaka kwa kutumia National Computer Emergency Response Team (TZ-CERT) imeendelea kukabiliana na majanga yatokanayo na Kompyuta na mifumo ya Mawasiliano”
“Katika kipindi cha Mwezi Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 Serikali kupitia TCRA imefanya tathmini na uchambuzi wa vihatarishi vya usalama katika mtandao na mifumo ya kompyuta kwa lengo la kubaini mapungufu yaliyopo dhidi ya mashambulio ya mtandao (cyber-attacks) ambapo
tahadhari za usalama (security alert) 875 na mashauri ya usalama mtandaoni (security advisories) 726 yalitolewa ili hatua stahiki ziweze kuchukulia kuimarisha usalama wa mtandao na mifumo”