Kocha Mkuu wa Simba SC Franco Pablo Martin amesema hana budi kutibu tatizo la kikosi chake kushindwa kupata matokeo katika viwanja vya ugenini, baada ya kufanya hivyo kwa michezo kadhaa msimu huu 2021/22.
Simba SC jana Jumapili (Mei 22) iliambulia matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Geita Gold FC iliyokua nyumbani Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kocha Pablo amesema tatizo la kikosi chake kushindwa kupata matokeo katika viwanja vya ugenini limeonekana kuwa kubwa, hivyo ni wajibu wake kufanya kazi ya ziada ili kulitatua, kama si msimu huu basi msimu ujao wa Ligi Kuu.
“Tumekua na tatizo la kushindwa kupata matokeo katika viwanja vya ugenini, sina budi kufanya kazi ya ziada kumaliza hili tatizo kwa kushirikina na wachezaji wangu, imekua kama tabia iliyozoeleka sasa.”
“Pamoja na mapufungu kadhaa yanayojitokeza, lakini hili tatizo linaniumiza mimi kama Kocha, ninaaminni hata kwa mashabiki linawaumiza pia, hivyo ni lazima tulitatue kama sio msimu huu, basi msimu ujao linapaswa kuondoshwa.” amesema Kocha huyo kutoa nchini Hispania.
Sare ya 1-1 imeendelea kuikwamisha Simba SC kufikia lengo lake la kuutetea Ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo, na kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikikisha alama 51.
Young Africans inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, imeendelea kuwa kileleni kwa kumiliki lama 63.