Benchi la Ufundi la Young Africans limekiri kuwa mchezo dhidi ya Simba SC hautakua rahisi kama inavyochukuliwa na Mashabiki wa klabu hiyo ambao msimu huu wamekua na muendelezo wa furaha kutokana na mambo kuwanyookea kwenye Ligi Kuu.

Simba SC itaikabili Young Africans kesho Jumamosi (Mei 28), katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kwenye mpambano wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Kocha Mkuu Nasredin Nabi amezungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Ijumaa (Mei 27), na kueleza namna ambavyo anauona mchezo huo, unaosubuiriwa kwa hamu kubwa.

Amesema upande wa maandalizi amejiandaa vyema kwa kutumia mbinu kadhaa ambazo anaamini zitawezesha kufanikisha lengo wanalolikusudia, lakini amekiri kwa kutanabaisha Simba SC ni timu nzuri na inatambua ubora wa mchezo kama wa kesho, hivyo anatarajia upinzani.

“Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wetu na Simba SC, hautakua rahisi kama unavyodhaniwa na mashabiki wa Yanga, ukweli ni kwamba wapinzani wetu wamejiandaa na wanafahamu ugumu na ubora wa michezo kama hii.”

“Huu ni mchezo mwingine kabisa hauna uhusiano wowote na michezo iliyopita kwa msimu huu ambayo tumecheza na Simba SC, najua mashabiki wanazungumza mengi kwa upande wao, lakini katika ufundi mambo yetu tunayajua wenyewe na tumejiandaa kweli kweli.” Amesema Kocha huyo kutoka nchini Tunisia.

Mshindi wa mchezo huo atacheza na mshindi wa mchezo wa Nusu Fainali ya Pili itakayounguruma keshokutwa Jumapili (Mei 29) jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kati ya Azam FC ya Dar es salaam dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Serikali:Kulipishwa vibao vya makazi si kosa'
Pablo: Utakua mchezo mgumu, tumejiandaa kushinda