Akizungumza Leo Jijini Dar es salaam alipozuru katika mto Mpiji akiwa ameambatana na wadau wa mazingira Kaimu Katibu Tawala Msaidizi anaesimamia huduma za Uchumi na Uzalishaji kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt Elizabeth Mshote amesema ni muhimu kwa jamii kuelimishwa ili kutunza kingo za mito huku akimpongeza Mkandarasi Kampuni ya MONDI LTD inayoshughulikia na usafishaji wa Mto.

Amepongeza jitihada za kutumia wataalam katika suala zima la kutekeleza mpango wa uboreshaji wa kingo za mito kwa kupanda miti itakayoendana na ekolojia ya eneo husika.

Katika ziara hiyo iliyolenga kufanya tathmini ya zoezi la upandaji miti  Mdau wa mazingira na mtaalamu wa miti Shadrack Kavenuke amesema ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa ushirikishwaji na uelimishwaji wa wananchi ni jambo muhimu huku akieleza mpango mzima wa namna ya zoezi la upandaji miti, na kufafanua kuwa zoezi la upandaji miti hadi kukua linaweza likachukua muda mrefu kuanzia miezi 3-6, hivyo ni muhimu mkandarasi au kikundi kinachpewa dhamana ya kusafisha mto kikazingatia hili.

Upi umuhimu wa kamati za mazingira kuangalia namna bora ya kuendelea kutunza miti mara mikataba ya usafishaji mito inapoisha.

Kwa kuzingatia uhalisia wa kinachofanyika sasa muda wa miezi miwili ya utekelezaji wa mipango kazi wa mazingira hauna tija. Maeneo yanayotakiwa kupandwa miti ni lazima yaainishwe sambamba na aina za miti inayotakiwa.

Aidha Mkurugenzi wa Kampuni ya MONDI LTD Bwana Francis Mondi anaesasfisha mto Mpiji ameomba kuongezwa muda wa Vibali vinavyotolewa ili uende sambamba na mapendekezo ya wataalam kwa kuwa Mkandarasi ndiye anawajibu kupanda miti na jukumu la kuitunza kwa kuzingatia muda wa kibali ambao ni miezi miwili tu.

Vilevile amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla kwa kufanikiwa zoezi la usafi na kuendelea kuhamasisha zoezi hilo kila mwisho wa mwezi na kuahidi kuendelea kuuunga mkono juhudi hizo kupitia usafishaji wa mto na kupanda miti ili kuhifadhi na kuboresha mazingira.

Naye Zamaradi Kawambwa mdau wa mazingira amehiza ushirikishwaji wa makundi yote hususani ofisi ya Serikali ya mtaa na Kata

Ifahamike kuwa zoezi la upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam ni muendelezo wa Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM ili kutunza Mazingira na kuufanya Mkoa huo uvutie wakati wote

Nachingwea kujenga kituo kukabiliana na Tembo
Mganga mkuu Wilaya ya Kigoma kuondolewa