Meneja wa Habari na Mwasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amewashukia baadhi ya wadau wa Soka wanaotumia kipindi hiki kutaka kuvuruga utulivu na amani ndani ya klabu hiyo, kwa kigezo cha kupoteza mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.
Simba SC ilipoteza muelekeo wa kutetea taji la ‘ASFC’ Jumamosi (Mei 28) kwa kukubali kufungwa 1-0 na Young Africans, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Ahmed Ally amewataka Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kuhakikisha wanaendelea kuwa kitu kimoja kama ilivyokua kabla hawajapoteza Ubingwa.
Amesema wanaotumia kipinfi hiki kupenyeza Chuki zao kwa kutoa maneno ya Kashfa na Kebehi, wanatakiwa kupuuzwa kwa hali zote, kwani Simba SC ina mipango yake kuelekea msimu ujao, baada ya kuanguka msimu huu.
Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe huo kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kwa kuandika: Nipo imara na naendelea na mapambano ?
Asanteni wote mnaonipa pole na asanteni wote mnaonikatisha tamaa niwaambie tuu ? hakuna kitakachonirudisha nyuma
Muhimu kwa wana Simba wenzangu ni kuwa makini nyakati hizi, wengi wataibuka kulaumu, kushauri na kuzodoa
Mwenye chuki atatumia matokeo haya kupenyeza chuki zake
Tuachane na hao watu hawana wanachotusaidia zaidi ya kutaka kutuvuruga
Tumeanguka msimu huu tunajipanga kurudi imara msimu ujao…
Namalizia sato wangu niliyotoka nao Mwanza?