Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele amemtakia kila la Kheri Kiungo Mshambuliaji Saido Ntibazonkiza aliyepewa mkono wa kwaheri Jangwani jana Jumatatu (Mei 30).

Saido alilazimika kuondolewa kambini juma lililopita baada ya kuonesha utovu wa nidhamu wakati wa maandalizi ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Simba SC.

Mayele ambaye amecheza na Kiungo huyo kutoka nchini Burundi msimu huu, amemtakia kheri na kumuombea mema.katika safari yake baada ya kuondoka Jangwani

“Ntibazonkiza Saidi Nakutakia kila la kheri najua sio mwisho wetu kwa sababu ulikuwa unamchango mkubwa kwangu ntaendelea kukukumbuka ntakumiss sana najuwa tutaendelea kuwasiliana lakini bado ulikuwa unaumuimu kwangu nakupenda kaka yangu” ameandika Fiston Mayele

Saido alisajiliwa Young Africans wakati wa Dirisha Dogo msimu uliopita akitokea Vital ‘O’ ya nchini kwao Burundi.

Serikali kununua silaha za raia kuepusha vifo holela
Wachezaji Simba SC wapumzishwa