Uongozi wa Simba SC umesitisha rasmi mkataba wa Kocha Franco Pablo Martin sambamba na Kocha wa viungo Danirl De Castro Reyes leo Jumanne (Mei 31).

Simba SC imetangaza maamuzi hayo baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha huyo kutoka nchini Hispania, ambaye alisifiwa kutokana na wasifu wake kuonesha aliwahi kupita Real Madrid.

Taarifa ya Simba SC iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii imeeleza kuwa, Kocha Msaidizi Seleman Matola amekabidhiwa jukumu la kuwa Kocha Mkuu wa muda hadi mwishoni mwa msimu huu.

Simba SC tayari imeshapoteza ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, huku Young Africans ikioewa nafasi kubwa ya kutwaa mataji hayo msimu huu 2021/22.

Kaduguda ashangaa maamuzi Simba SC
Hukumu ya Sabaya yasogezwa mbele