Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake leo Juni Mosi, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Moshi Kilimanjaro kwa tuhuma za makosa ya uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa Mwendesha mashataka wa Serikali Tumaini Kweka amesema Lengai Ole Sabaya, Nathan Msuya, Sylvester Nyegu, Antheo Boniface Assey na John Aweyo wanashtakiwa kwa makosa saba ya uhujumu uchumi.

Makosa mengine ni pamoja na kuongoza genge la uhalifu, kutenda kinyume na mamlaka yake, kujihusisha na vitendo vya rushwa na utakatishaji fedha.

Awali Wakili upande wa utetezi Hellen Mahuna ameiomba Mahakama hiyo kutenda haki kwa madai kuwa wateja wake na Mahakama ya Arusha haikupata kibali halali cha kuwatoa washtakiwa gereza la Kisongo  Arusha na kuwapeleka gereza la Karanga Moshi.

Hata hivyo Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakamu ya hakimu mkazi Moshi Kilimanjaro Salome Mshasha ameahirisha kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2022 hadi Juni 7, 2022 itakapotajwa tena.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 2, 2022   
Maelfu ya vijiji kuunganishiwa umeme 2022/23