Leo June 02, 2022, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, liliahirishwa kwa muda wa nusu saa baada ya Waziri wa Nishati Januari Makamba na Naibu wake, Stephen Byabato kutokuwepo bungeni katika muendelezo wa majadiliano kuhusu upitishwaji wa Bajeti ya wizara hiyo.

Muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Bunge kuliahirisha Bunge kutokana na hoja hiyo ya kutokuwepo kwa viongozi hao, Waziri wa Nishati, Januari Makamba alirejea Bungeni na kikao kuendelea.

Makamba na Naibu wake hawakuwepo Bungeni wakati wabunge wakichangia hoja yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/23 aliyoiwasilisha Juni mosi.

Taifa Stars kuifuata Niger leo
Wananchi wataharuki biashara ya vidole