Mdau wa Soka la Bongo Jemedari Said Kazumari ameipinga Kampeni ya ‘Nani Zaidi’ iliyozinduliwa rasmi jana Alhamis (Juni 02) na klabu za Simba SC na Young Africans chini ya uratibu wa Azam Media.

Simba SC na Young Africans zilithibitisha kushiriki katika kampeni hiyo itakayowahusisha Mashabiki na Wanachama wa klabu hizo Kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki, kupiga kura kupitia huduma za kutuma na kupokea simu mtandaoni.

Jemedari ameipinga Kampeni hiyo akiwa katika Kipindi cha SPORTS HQ cha EFM leo Ijumaa (Juni 03) kwa kusema: “Kampeni ya NANI ZAIDI iliyoanzishwa na vilabu vya Simba na Yanga ni namna mpya ya kudumaza akili za uwekezaji katika soka la Tanzania.”

“Wanataka kununua kiwanja sio kujenga kiwanja…”

“Siafikiani na hizi kampeni wakati tayari shabiki ananunua jezi, analipia king’amuzi na tiketi kwa uwepo wake uwanjani kwanini wanataka buku buku zao tena?”

“Kitendo cha viongozi wa Simba kwenda Qatar na kwingineko kutafuta viwanja mara baada ya kusaini kampeni za NANI ZAIDI inaonesha namna gani hakukuwa na mpango wa kujenga kiwanja tangu mwanzo…”

“Vilabu ndani ya miaka 80 vinaenda na kurudi pale pale hawajui namna ya kuwekeza…”

Mashabiki wanapata nini? Hapa sports HQ ukimwamwambia mtu aweke 1000 atapata 500k mpaka 2M
“Sasa kwenye NANI ZAIDI mashabiki wanapata nini?”

“Simba na Yanga ni taasisi zenye nguvu na ushawishi zaidi Afrika Mashariki na Kati lakini ndio taasisi masikini zaidi ambazo hazijimudu” kwa gaharama.

Stars mguu sawa kuivaa Niger, Samatta afunguka
Fiston Mayele kutimka Young Africans