Beki wa Klabu ya Portsmouth ya England Haji Mnoga ametoa wito kwa wachezaji wenye asili ya Tanzania, kufikiria kurudi nyumbani na kuitumikia Timu ya Taifa ya nchi hiyo ‘Taifa Stars’. 

Mnoga ametoa wito hiyo kwa Watanzania wanaocheza soka nje ya nchi, akiwa katika kambi ya Taifa Stars akijiandaa na mchezo wa kusaka Tiketi ya kucheza ‘AFCON 2023’ dhidi ya Algeria keshokutwa Jumatano (Juni 08). 

Beki huyo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Stars kilichoanza dhidi ya Niger juzi Jumamosi (Juni 04), amesema ni fahari kuitumikia Taifa Starts ambayo inahitaji usaidizi wa wachezaji wenye uzoefu, ili kufanikisha lengo ya kuwa timu bora barani Afrika na Duniani kwa ujumla. 

Amesema kwake haikuwa rahisi kufanya maamuzi ya kurejea nyumbani Tanzania, lakini alivyofanya hivyo alijua umuhimu wake, na leo amekua sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kinachosaka Tiketi ya AFCON 2023.  

“Ulikuwa uamuzi mgumu kwa sababu nilizaliwa Uingereza. Lakini, kwangu, niliona fahari zaidi kuichezea Tanzania.” 

“Inawezekana kuifanya Tanzania kuwa moja ya mataifa hatari kwenye mpira wa Afrika, Natumai kaumua kwangu kuichezea Tanzania kutaongeza msukumo kwa wachezaji wengine na kuona kuwa wana kila sababu za kuamua kulitumikia taifa lao na huo ndio uzalendo,” amesema Mnoga. 

Mara ya kwanza Mnoga aliitwa Taifa Stars wakati wa michezo ya kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati, mwanzoni mwa mwaka huu.  

Young Africans yamkana Cesar Manzoki
Hatuuzi vidole: Serikali Zimbabwe