Idadi ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa virusi vya Uviko-19 imeongezeka hadi kufikia 161 ikilinganishwa na maambukizi 68 kwa kipindi cha Aprili 2 hadi Mei 4, 2022.

Taarifa ya Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale, imesema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 137 na kwamba katika kipindi cha miezi miwili mfululizo hakuna kifo kilichoripotiwa.

Idadi ya maambukizi katika kipindi cha Mei 5 hadi Juni 3, 2022 inaonesha Mkoa wa Dar es Salaam una visa 130, Arusha 10, Mwanza 5, Shinyanga 4, Mtwara 3, Dodoma 2, Mara 2, Morogoro 1, Simiyu , Katavi 1, Mkoa wa Kilimanjaro 1 na Mbeya 1.

Serikali nchini imeendelea kutoa huduma ya chanjo ya uviko-19 ili kuwezesha wananchi kupata kinga na Wizara bado inawasisitiza wananchi kupata na kukamilisha dozi ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

Majaliwa ang'aka pikipiki za Maafisa Ugani
Hofu yatanda kukamatwa bunduki 200, risasi 3,000