Polisi nchini Kenya katika Kaunti ya Kirinyaga inamsaka aliyekuwa mfungwa kwa amemuua mama yake kwa kumkatakata na mapanga.

Mwanamume huyo ni mmoja wa wafungwa 3908 wa makosa madogomadogo ambao walisamehewa na Rais Uhuru Kenyatta katika sherehe za siku ya Madaraka Juni 1, 2022.

Insemekana sababu za magombano yao ni kile kinachokisiwa kuwa ni mzozo wa shamba ambapo mwanamume huyo alimuua mamake kwa kumkatakata kisha kukimbilia mafichoni.

Mtuhumiwa huyo alimuua mama yake Grace Muthoni Ndambiri, bafuni katika kijiji cha Njoga mnamo Jumapili, Juni 12, na kukimbilia mafichoni.

Majirani ambao walifika kusaidia baada ya kusikia kelele za kuomba msaada walikuta mwanamke huyo mwenye umri mkubwa akiwa amelala kwenye kisima cha damu na kutoa ripoti polisi.

Mkuu wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Mwea Mashariki, Daniel Kitavi alisema kuwa maafisa wake walikuta mwili wa mama huyo ukiwa katika nyumba kuu, wakautoa na kuupeleka katika Makafani ya Kibugi.

“Mwanamke huyo alishambuliwa vibaya sana na alikuwa na majeraha mabaya ya kukatwakatwa kichwani,” Kitavi alisema.

“Mwanamume huyo ambaye aliachiliwa kutoka gerezani na Rais amekuwa akitaka sehemu ya ardhi ya familia kutoka kwa mama yake na wawili hao wamekuwa wakigombana kwa muda mrefu, tunashuku mwanamume huyo alimuangamiza mwanamke huyo mzee alipokata kuridhia shinikizo zake,” Kitavi aliongeza.

Kitavi alisema kuwa mwanamke huyo alikuwa akiishi na mwanawe baada ya mume wake kufariki Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa polisi, maafisa wake pamoja na wakazi walikuwa wakimtafuta mshukiwa mabaye alitoroka punde tu baada ya kumwangamiza mamake.

KKKT Konde mgogoro usioisha, Polisi yaingilia
Urusi yasambaratisha ngome muhimu ya Ukraine, Rais anena