Serikali ya Uingereza leo Juni 14, 2022 inapanga kuendelea na kusafirisha maelfu ya waomba hifadhi nchini Rwanda, kwa ajili ya kushughulikia na kuwapatia makazi mapya baada ya Mahakama kuzuia rufaa mbili za mpango huo wenye utata hapo jana Juni 13, 2022.

Uamuzi huo umefanywa na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa, na ulikuja baada ya Mahakama Kuu kushindwa kupitisha zuio la kupinga mpango huo uliopendekezwa wiki iliyopita na Jaji Rabinder Singh, kusema maombi ya msamaha wa muda yatahitaji kuzingatiwa kutokana na majibu ya kesi.

“Tunatazamia kuwa maombi ya msamaha yatazingatiwa kutokana na kesi baada ya kesi ambazo zitatupa majibu ya nini kinahitajika kuchukuliwa hatua na kwa mazingira ya namna gani na hii ni kwa kesi zote za namna hii,” alisema Jaji Singh.

Care 4 Calais, moja ya vikundi vya misaada vilivyohusika katika rufaa hiyo, ilisema watu 23 ambao walikuwa wamepangwa kuondoka kwa ndege ya kwanza leo Juni 14, 2022, tiketi zao zilifutwa na hivyo kusababisha baadhi yao kukosa safari.

“Sasa baada ya uamuzi huo wa kufuta hizo tiketi umefanya watu wanane waliopangwa kuondoka kukosa safari lakini msemaji wa kikundi alitarajia kwamba rufaa binafsi za abiria kuhusu kughairi tiketi za safari ingefaulu,” ilisema sehemu ya taarifa ya kikundi hicho cha msaada.

Kwa mujibu wa data zilizochapishwa na Ofisi ya Mambo ya Ndani ya Uingereza, zinasema mwaka 2021, zaidi ya watu 28,500 walifika nchini humo kwa boti ndogo wakitokea maeneo mbalimbali, idadi ambayo inazidi ile ya mwaka 2020 ya watu 8,466.

Hata hivyo, majibu ya Wataalamu wa haki za Kimataifa na makundi yanayowakilisha wanaotafuta hifadhi wanasema, sera hiyo yenye misimamo mikali inakiuka ahadi ya Uingereza kwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi ya mwaka1951.

Sera hiyo inaelekeza kuwa watu wenye uhitaji na wanaotafuta hifadhi wanatakiwa kutopelekwa kwa nguvu katika maeneo yasiyo salama, kitu ambacho kinaumngwa mkono na Umoja wa Mataifa (UN).

Macho na masikio Dodoma, bajeti mpya itakidhi hali?
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 14, 2022