Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewatupia Dongo mashabiki wa Klabu ya Simba nchini huku akimsifia Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele kuwa mchezaji huyo anafanya nchini vizuri na amekuwa maarufu kuliko hata baadhi ya viongozi.

Mwigulu ambaye ni shabiki kindakindaki wa Young Africans amesema hayo jana Jumanne (Juni 14) wakati akimalizia kuwasilisha hoja ya mapendekezo ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 Bungeni jijini Dodoma.

“Nakupongeza Mheshimiwa Anthony Mavunde wewe ndio ulikuwa Mwenyekiti wa kuisaidia Young Africans ikiwa na mapito. Nampongeza GSM kwa kurejesha furaha ya wananchi hasahasa kwa udajili wa Fiston Mayele.

“Mayele amekuwa maarufu kuliko Makatibu wenezi wa baadhi ya vyama vya Siasa. Nawapongeza sana na marafiki zangu klabu ya Simba kwa kuwakilisha vyema kwenye mashindano ya Kimataifa, wananijua mara zote kimataifa tuko pamoja, siwezi kukana Bendera ya Taifa langu kwa ajili ya utani wa jadi,” alisema Mwigulu.

Ikumbukwe kuwa, Mayele ndiye mchezaji mwenye mabao mengi kwa sasa kwa wachezaji wa Young Africans lakini anashika nafasi ya pili kwa wafungaji wa Ligi Kuu mpaka sasa akiwa na jumla ya mabao 14 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na George Mpole wa Geita Golf FC mwenye mabao 15.

Wawili hao ndio wanatajwa kuwania kiatu cha ufungaji Bora wa Msimu wa 2021/2022 ambayo bado mizunguko mine ili kutamatika kwa ligi hiyo ambapo Yanga wanahitaji pointi tatu tu kutangaza ubingwa huku wakiwa na mechi nne mkononi mpaka sasa.

Simba SC: Hatuna mpango na Luis Miquissone
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 15, 2022