Urusi imewapiga marufuku kuingia nchini humo raia 49 wa Uingereza, wakiwemo maafisa wa ulinzi na Waandishi wa Habari mashuhuri na Wahariri kwa kujihusisha kwa makusudi kusambaza habari za uwongo na za upande mmoja kuhusu Urusi na matukio ya Ukraine na Donbass.

Miongoni mwa waandishi wa habari waliopigwa marufuku ni pamoja na Shaun Walker wa The Guardian, Gideon Rachman wa The Financial Times na mwanaharakati Mark Galeotti.

Serikali ya Uingereza imekuwa imekuwa ikiiunga mkono Ukraine baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin kupeleka majeshi yake Ukraine Februari 24.

Urusi pia imewapiga marufuku mamia ya wabunge wa Uingereza, huku Wizara ya mambo ya nje ikitangaza mpango wa kupanua orodha hiyo, inayojumuisha wanachama 29 wa vyombo vya habari na watu 20.

Wahariri waliopigwa marufuku ni kutoka Shirika la Habari la Uingereza (BBC), The Financial Times na The Guardian.

Adel Zrane: Ninafahamu kinachoendelea Simba SC
Azam FC yaingilia mipango Simba SC