Wafanyakazi wa sekta afya Zimbabwe, wameanza mgomo kupinga masharti ya malipo kutokana na mzozo mpya wa kifedha nchini humo kwa kufikisha ujumbe wao kwa serikali ulio katika mabango nje ya ofisi za Baraza la Huduma za Afya katika moja ya hospitali kubwa nchini humo.
Wamesema, mpango huo mpya unaotokana na kuporomoka kwa uchumi unawapa ukakasi na kwamba wamekuwa wakishuka kiufanisi, huku Askari wa kutuliza ghasia waliwekwa kwenye uwanja wa hospitali hiyo, kitendo kilichosababisha wagonjwa kukosa tiba.
“Wafanyakazi wa afya wanalipwa ujira mdogo, Wanajitahidi kujikimu na tuna mahitaji mengi sasa kwa namna hii haifai tunashuka kiutendaji kitu kitakacholeta madhara,” alisema muandamanaji Kiongozi wa Muungano wa Sekta ya Afya, Tapiwanashe Kusotera.
Wanasema wao kama Wauguzi nchini Zimbabwe wanapata dola za Zimbabwe 18,000 kwa mwezi, ambazo ni sawa na takriban dola 55 (euro 52) huku Walimu wakipata takriban $75 kwa mwezi.
“Bodi yetu ya Huduma za Afya ambayo ni mwajiri wetu na Wizara ya Afya wamekataa kabisa kuzungumza na wafanyakazi hao,” alisema Mkuu wa Chama cha Wauguzi nchini, Enock Dongo.
Serikali, juma lililopita ilisema kwamba itaongeza mishahara maradufu ya watumishi wote wa umma, lakini Dongo alisema hakuna ofa rasmi iliyotolewa mpaka sasa na Juni 20, 2022 Walimu walitangulia kuitisha mgomo wa siku tano, kulingana na taarifa ya chama cha walimu.
“Hatuwezi kuendelea kuwa aibu kwa jamii yetu kwa sababu ya umaskini ambao serikali inauchukulia kuwa sehemu ya maisha yetu ya kufanya kazi,” iliandika.
Uchumi wa Zimbabwe uko katika mgogoro mkubwa, ikiwa ni pamoja na kujiondoa kwa wafadhili wa kimataifa kwa sababu ya madeni yasiyo endelevu.
Mfumuko wa bei ulifikia 131% mwezi Mei, na kufufua kumbukumbu za mfumuko wa bei zaidi ya muongo mmoja uliopita. Bei zilikuwa zikidorora na benki kuu ilitoa noti ya dola trilioni 100 mwaka 2008, ambayo imekuwa bidhaa ya ushuru.
Uvamizi wa Ukraine umesababisha hali kuwa mbaya zaidi, kwani Urusi ndiyo msambazaji mkuu wa ngano na kemikali zinazotumika katika kilimo cha Zimbabwe.