Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal Pape Ousmane Sakho amewashukuru Mashabiki wa Klabu ya Simba SC, kwa upendo waliomuonesha wakati wote tangu alipojiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu 2021/22.

Sakho ametoa shukurani hizo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, huku akiwataka Mashabiki kuendelea kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki ambacho Simba SC, imemaliza msimu bila ubingwa.

Kiungo huyo amewaahidi Mashabiki kuwa, msimu ujao utakua na furaha, kwani anaamni Simba SC itapambana kwa nguvu zote na kurudisha heshima ya Ubingwa.

Sakho ameandika: “Msimu unaisha hivi karibuni, ninachukua nafasi hii kusema ASANTENI mashabiki wa Simba SC kwa juhudi zenu zote, kunitia moyo na upendo na sapoti mliyonipa tangu mwanzo. Mlikuwepo siku zote katika nyakati ngumu na za furaha, Mlikuwa hodari na wenye nguvu. jasiri pia mambo yalipokuwa mabaya…”

“Tutarudi kwa nguvu zaidi kuwafanya mtabasamu tena, mfahamu tu kwamba nawapenda kwa moyo wangu wote na sitasahau upendo ambao timu hii nzuri ilinipa. Tutaonana hivi karibuni??♥️”

Sakho alisajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu huu 2021/22, akitokea klabu ya Teungueth FC ya nchini kwao Senegal.

Juni 30 Young Africans wana jambo lao
Rais Samia amtaja Mama Mkapa kwenye safari yake ya siasa