Mwanasheria wa Klabu ya Young Africans Patrick Simon, amesema kuanzia Juni 30 klabu hiyo itaendelea na mpango wa kuwatambulisha wachezaji wapya wa klabu hiyo.

Young Africans tayari imeshamtambulisha Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Lazarius Kambole, huku kukiwa na tetezi huenda klabu hiyo ikawatangaza wachezaji wengine wawili wa Kimataifa.

Kambole amejiunga na klabu hiyo ya Jangwani, baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, mwishoni mwa msimu wa 2021/22.

Simon ambaye aliwahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo amesema: “Nitafuteni Juni 30, kuna jambo nitawaambia, endeleeni kusubiri maana tumejizatiti kuendelea kutangaza usajili wetu wa wachezaji tutakaokuwa nao msimu ujao.”

Young Africans inahusishwa na mpango wa kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka Burkina Fasso na klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast Stephen Aziz Ki, sambamba na Bernard Morrison aliyeachwa na Simba SC.

Okrah amaliza vibaya Ghana, kutua Dar es salaam
Sakho awatuliza Simba SC, aahidi makubwa 2022/23