Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana na klabu ya Bechem United Augustine Okra, amewaomba radhi Viongozi wa Chama cha Soka nchini humo, Viongozi wa Klabu yake pamoja na Mashabiki kwa ujumla, baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa Fainali wa kombe la FA.
Bechem United ilipoteza mchezo huo wa Fainali kwa kufungwa 2-1 na Accra Herts Of Oak Jumapili (Juni 26), ukiwa mchezo wa mwisho wa kufunga rasmi msimu wa 2021/22 nchini Ghana.
Okrah anayehusishwa na mpango wa kusajiliwa na Mabingwa wa zamani wa Tanzania Bara Simba SC, alioneshwa kadi nyekundu, baada ya kupinga maamuzi ya mwamuzi wa pembeni, huku wengine wakidai alimsukuma na ndipo mwamuzi wa kati alipochukua maamuzi kumuadhibu.
Mshambuliaji huyo ameutaka Uongozi wa Chama cha Soka nchini Ghana umsamehe kwa kosa hilo na anajutia kufanya hivyo kwani halikua kusudio lake, na siku zote amekua ni mtu mwenye nidhamu uwanjani.
Upande wa Viongozi wa klabu ya Bechem United, Okrah amewataka msamaha, kwani anaamini adhabu iliyomkuta ilisababisha kwa kiasi kikubwa kwa timu yake kupoteza mchezo huo wa Fainali, hali kadhalika kwa wadau wa soka nchini Ghana nao amewahimiza wamsamehe kwani amefanya makossa kama binadamu.