Rais Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la Fistula kwa watoto wa mwaka 4 hadi 12 linasababishwa na ubakaji.

Rais Samia amesema hayo alipotembelea hospitali ya CCBRT na kukagua wodi ya wanawake wenye matatizo ya Fistula.

Amesema inakadiriwa wanawake 12000 Hadi 18000 wana tatizo la fistula huku watoto wakikadiriwa kuwa na miała 4 hadi 12 wakiwemo katika orodha hiyo.

“Ndugu zangu watanzania, Tatizo hili la ubakaji ambalo kwa kiasi kikubwa tunalifumbia macho kwenye jamii hatuwapeleki kwenye combo via Sheria tunakosea.”

Ameongeza, “kwa hiyo niwaombe sana ndugu zangu tupunguza sana idadi hiyo ya wanawake wanaoishi na fistula nchini kwa kuepuka yanayoweza kuepukika ambayo ni Ndoa za utotoni, ubakaji, mimba za utotoni na mila potofu,”

Rais Samia alikua mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Jengo jipya la mama na mtoto hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam, Leo Julai 5, 2022.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Julai 06, 2022
Ummy Mwalimu:Barakoa bado lazima