Serikali, imewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa (Mipango), Uratibu na Serikali za Mitaa, Maafisa Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji na Waweka Hazina wa Halmashauri kutekeleza kwa tija na ubunifu katika kusimamia mipango ya bajeti na uwajibikaji. 

Naibu Katibu Ofisi ya Rais ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt.  Grace Magembe (afya), ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kwa maafisa. 

“Kila kinachofanyika ni lazima kila mmoja ahakikishe amefanya kwa nafasi yake badala ya kuja na visingizio maana mwisho wa siku wote tutawajibika kwa utendaji mzuri au mbaya wa taasisi,” amesema.

Katika kikao hicho, kilichoanza kufanyika hii  leo Juni7, 2022 Jijini Dodoma pia watumishi hao wamehimizwa kusimamia kwa karibu ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma, ili ziweze kutekeleza miradi iliyopangwa na Serikali . 

“ Simamieni nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kuchukua hatua kwa wakati kwa watendaji watakaoshindwa kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma na taaluma zao,” amesema Dkt. Magembe

Katika hatua nyingine, maafisa hao wametakiwa kuhakikisha wanasimamia umalizaji wa miradi kwa wakati na viwango, kwani Serikali haitavumilia miradi viporo.

Dkt. Magembe amesema, utendaji wa sekretariati za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa utapimwa kwa vigezo vya upelekaji wa fedha za miradi asilimia 40 kwa 60 kwenye miradi ya maendeleo.

Tanzania ndani ya “IDA SUMMIT” Senegal
Simbachawene kuongoza harambee kampeni GGM KILI CHALLENGE 2022