Baada ya Simba SC kukamilisha usajili wa Kiungo kutoka nchini Nigeria Victor Akpan, na kumtambulisha kwa Mashabiki na Wanachama jana Jumapili (Julai 10), Kocha Mkuu wa Coastal Union Juma Mgunda amesema klabu hiyo ya Msimbazi imepata mchezaji wa maana.

Akpan amesajiliwa Simba SC akitokea Coastal Union ambayo aliitumikia kwa msimu mmoja (2021/22), na kuwa sehemu ya kikosi kilichocheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Young Africans jijini Arusha Jumamosi (Julai 02).

Mgunda amesema kwa asilimia kubwa mafanikio ya Coastal Union kwa msimu uliopita yalichangiwa na Kiungo huyo, ambaye ana uhakika atafanya mazuri zaidi akiwa Simba SC, kutokana na nafasi ya klabu hiyo kucheza Kimataifa msimu ujai (2022/23).

“Nikiri katika wachezaji ambao wameipa mafanikio klabu ya Coastal Union japo ni madogo kwa msimu uliopita, Akpan ni mmoja ya wachezaji hao, alilikua nguzo kwenye kikosi changu, wapo wengine ambao walifanya vizuri lakini uwezo wa huyu mchezaji ulinisaidia sana,”

“Binafsi ninamuombea dua njema kwenye Maisha yake mapya huko Simba SC, nina uhakika atapata nafasi kubwa zaidi ya kucheza kutokana na klabu iliyosamsjili kuwa na fursa ya kushiriki michuano ya kimataifa.”

“Unapomzungumzia mchezaji humzunguzii yeye kama yeye, unamzungumzia kwa nafasi anayocheza, Akpan ni mchezaji ambaye katika aneo analocheza anaweza kuimudu nafasi yake vizuri hasa mnapohitaji kitu ama mnapotaka kujilinda, ni moja kati ya wachezaji wenye mchangu mkubwa sana.” Amesema Mgunda

Akpan amekua mchezaji watatu kutambulishwa Simba SC akitanguliwa na Mshambuliaji Moses Phiri kutoka Zambia pamoja na Mshambuliaji wa Tanzania Habib Kyombo aliyetambulishwa Jumamosi (Julai 09).

Wanafunzi wafa kwa kukosa hewa ndani ya 'School Bus'
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Julai 11, 2022