Mara baada ya mamia ya waandamanaji kutata Rais wa Sri Lanka na Waziri Mkuu wa nchi hiyo kujiuzulu, Vyama vya kisiasa nchini humo vimekutana kukubaliana kuhusu serikali mpya.
Waandamanaji hao, walivamia makazi ya Viongozi hao na kuchoma moto nyumba ya Waziri Mkuu katika hatua ya kuchukizwa kuhusu mzozo wa kiuchumi.
Hata hivyo, Mbunge wa upinzani M. A. Sumathiran amesema vyama vyote vya upinzani kwa Pamoja vinaweza kupata kwa urahisi wanacham 113 wanaohitajika kuonyesha wingi wa viti bungeni, ambao watamuomba Rajapaksa kutangaza serikali mpya na kisha kujiuzulu.
Waandamanaji, walivamia nyumbani kwa rais Gotabaya Rajapaksa na makaazi ya Waziri mkuu, wamesema wataendelea kubaki hapo hadi pale viongozi hao watakapojiondoa rasmi madarakani.