Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi ameupongeza Uongozi wa klabu hiyo kwa kufanya usajili unaokidhi matakwa ya Benchi la Ufundi kuelekea Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Young Africans itaanza msimu ujao 2022/23 ikiwa na kazi kubwa ya kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ pamoja na uwakilishi wa Tanzania Kimataifa.

Kocha Nabi ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni baada ya kumaliza majukumu yake kwa msimu wa 2021/22, amesema Uongozi wa Young Africans umefanya kazi yake ipasavyo kwa usajili wa kuzingatia sifa za wachezaji alizozipendekeza.

Amesema katika safu ya kiungo ana uhakika mambo yataendelea kuwa mazuri kutokana na wachezaji waliopo na wengine walioongezwa akiwemo Kiungo kutoka Burundi ya Bigirimana, ambaye amedai uzoefu wake utakua msaada mkubwa kikosini mwake.

“Tuna Sure boy, Aucho, Feisal na Mauya ubora mkubwa wa hawa watu wanne Bado tunaongeza na Nguvu ya Bigirimana, ni mchezaji mzoefu anayejua kutengeneza ugumu eneo la kiungo, Roho yangu sasa imetulia kwa huu usajili.” Amesema Nabi

Young Africans tayari imeshawatambulisha Lazarous Kambole kutoka Zambia, Bernard Morrison kutoka nchini Ghana pamoja na Bigirimana ambaye aliwahi kucheza soka katika Ligi Kuu ya England akiwa na klabu ya Newcastle United.

Dickson Mhilu: Bado nipo sana Kagera Sugar
Simba SC kumtambulisha mwingine leo Jumatatu