Ajali iliyohusisha magari madogo mawili, imesababisha vifo vya watu watano na wengine 11 wamejeruhiwa iliyotokea eneo la Magereza nje kidogo ya mji na Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mji wa Bariadi, Somanda Emmanuel Constantine amethibitisha Hospitali hapo kupokea miili ya watu wanne na majeruhi wanne.

“Majeruhi tuliowapokea wamepata majeraha kwenye migongo na hali zao zinaendelea vizuri na hadi sasa wanaendelea kupatiwa matibabu” amesema.

Gavana wa zamani ahukumiwa kwa mauaji

Ndege zisizo na rubani kupima ardhi Nchini

Magari hayo ya abiria aina ya Toyota pro box na Toyota wish, ambayo hufanya safari zake kati ya mji wa Bariadi na Lamadi wilayani Busega yaligongana uso kwa uso.

Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharura wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Dkt. Seleman Athuman amesema alipokea amjeruhi wanane na mmoja alifariki wakati akitibiwa na kufanya idadi ya vifo kuwa watu watano.

Ajali hii, inatokea ikiwa ni siku 13 tangu kutokea kwa ajali nyingine ya gari aina Toyota wish katika eneo la Luguru wilaya ya Itilima mkoani humo, kwa kuua watu watano kujeruhi wengine watano.

Gakumba: Meddie Kagere bado yupo sana Simba SC
Huenda ikawa zamu ya Okrah Simba SC