Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana, Augustine Okrah huneda atambulishwa Simba SC ndani ya saa 48 zijazo, baada ya kuwasili Dar es salaam, akitokea nchini kwao.

Simba SC imekuwa ikihusishwa na nyota huyo aliyeaga Bechem United ya nchini kwao Ghana, tangu kufunguliwa kwa Dirisha la Usajili kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Taarifa zinadai kuwa nyota huyo ametua nchini tangu jana Jumanne (Julai 12) asubuhi, na ameshapiga picha za utambulisho na jezi ya timu hiyo hivyo kinachosubiriwa ni utambulisho kutoka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za timu hiyo.

Okrah ana thamani ya Euro 150,000 (Sawa na Shilingi million 352, 227, 000) kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market unaohusika na thamani za wachezaji duniani.

Mghana huyo alikuwa kwenye kiwango bora msimu uliopita ambapo alifanikiwa kufunga magoli 14 akishika nafasi ya tatu ya Frank Etouga wa Asante Kotoko aliyeshika nafasi ya pili akifunga magoli 21 na Yaw Annor wa Ashanti Gold ambaye alifunga magoli 22.

Klabu ya Bechem United iliyokuwa inamiliki Okrah, ilimaliza nafasi ya tatu kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Ghana ikiwa na alama 54, huku ikikifanikiwa kufika Fainali ya Kombe la FA na kupoteza dhidi ya Accra Haerts Of Oak.

Nyota huyo amewahi kuzitumikia Al Hilal na Al Merrikh za nchini Sudan, Hacken ya Sweeden, Smouha ya Misri na NorthEast United ya India.

Pia ameezitumikia timu za Bechem United na Asante Kotoko katika nyakati tofauti na ameichezea timu ya Taifa ya Ghana mara mbili.

Okrah ambaye ni mzaliwa wa mji wa Obuasi huko Ghana ana umri wa miaka 28 na anamudu kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji wa katikati na akitokea kulia na kushoto.

Inasemekana wakati yuko kwenye safari ya kuja Tanzania viongozi wa Chama cha Soka cha Ghana walimuomba arejee akiichezeee timu ya taifa kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya CHAN lakini nyota huyo aligoma kurejea.

Watano wafa ajalini Simiyu
Gavana wa zamani ahukumiwa kwa mauaji