Mshambuliaji wa Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga, Fiston Mayele bado yupo mapumzikoni DR Congo, lakini ametuma salamu kwa Simba akiwaambia kwamba ameipata dawa yao na ataionyesha kwenye mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Agosti 13 kuzindua msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2022-2023.

Mayele aliyemaliza msimu uliopita na mabao 16, bao moja nyuma ya George Mpole wa Geita Gold, ndiye aliyefunga bao pekee lililoizamisha Simba kwenye mechi ya Ngao ya Jamii ya msimu huo, lakini akashindwa kufunga katika mechi tatu zilizofuata za watani wa jadi mbili za Ligi Kuu na moja ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Akitambua kuwa msimu huu atakutana tena na Simba kwenye mechi ya Ngao, Mayele alisema katika mechi ya msimu uliopita hakupata maandalizi ya kutosha, licha ya kuwatungua, lakini safari hii anaamini atakuwa na muda mzuri wa kujifua na timu na Simba itapata tabu sana siku hiyo.

Azam FC yafunguka umafia walioufanya Ivory Coast
Sakata la Manzoki, Simba SC yaomba msaada FIFA