Uongozi wa Azam FC umefichua siri ya Usajili wa Kiungo Mshambuliaji Tape Edinho ambaye alitua Chamazi mwezi uliopita akitokea nchini kwao Ivory Coast.

Azam FC imemsajili kiungo huyo katika mipango yake kuelekea msimu wa 2022/23, ambapo wamejizatiti kufanya vizuri kwenye michuano ya ndani na nje ya Tanzania.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria ‘Zakazakazi’ mapema leo Jumatano (Julai 20), alifichua mpango wote wa usajili wa Tepe, akidai alikua akiwindwa na ASEC Mimosas kama mbadala wa Stephen Aziz Ki aliyetua Young Africans.

“Aziz Ki alishawaambia ASEC Mimosas kuwa hatobaki, ataondoka baada ya misimu yake miwili kukamilika. ASEC wakaanza kuhangaika kumchukua Tape Edinho kwenda kuchukua nafasi ya Aziz Ki”

“Walikuwa wanahangaika na replacement wakaenda kwa Tape, wakati huo Tape anadili la kwenda Ufaransa, kwa hiyo Tape aliwakatalia ASEC Mimosas akasema anataka kwenda Ufaransa”

“Sisi tumetengua ile ya kwenda Ufaransa (Tape Edinho akaja hapa, yawezekana ASEC mpaka sasa hivi wanajua Tape yuko Ufaransa, wanadhani Azam FC ni timu ambayo iko Ufaransa” amesema Zakazakazi

IGP Wambura, Balozi Sirro waapa Ikulu
Fiston Mayele aichimba mkwara Simba SC