Wakati Simba SC ikiendelea kukiimarisha kikosi chao kwa kujiandaa Kambini Ismailia-Misri, Usajili wa Klabu hiyo umepondwa na kutazamwa kama tatizo ambalo litakwenda kuwaumiza Mashabiki na Wanachama wake kwa mara ya pili Mfululizo msimu ujao 2022/23.
Simba SC ilipoteza Ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Tanzania ‘ASFC’ na kushindwa kufikia malengo ya Michuano ya Kimataifa kwa msimu wa 2021/22 (Kombe la Shirikisho Barani Afrika).
Usajili wa Klabu hiyo ambao unaonekana kama suluhisho la kurejesha furaha kwa Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo, umepondwa na Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na Klabu ya Mtibwa Sugar Meck Mexime.
Mexime ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Kituo cha Kukuza na Kulea vipaji kwa Vijana cha Cambiaso, amesema Simba SC imeendelea kufuga tatizo kwenye kikosi chao, na haamini kama usajili uliofanywa katika kipindi hiki kama utaweza kusaidia.
Amesema asilimia kubwa ya wachezaji ambao wanaendelea kuwa sehemu ya kikosi ni wale ambao walishindwa kuipa matokeo klabu hiyo ya Msimbazi, kutokana na kukosa sifa za ushindani.
“Simba SC, hawajui hata wanalofanya, kuna wachezaji pale rundo, msimu uliomalizika hakuna la maana walilolifanya, wamechoka na wamezeeka na viongozi wanalijua hilo ila wanavigugumizi, eti kuvunja mikataba wanashindwa, ni ubabaishaji tu kwenye soka”
“Kuwaacha wachezaji waliokosa mipango waendelee kuwa sehemu ya kikosi ni hatari sana, hawa ndio huwa wanageuka wachawi kuroga wachezaji vijana wanao perform ili wapate nafasi ya kucheza,”
“Nimecheza mpira nayajua haya, siongei kufurahisha genge hapa , Simba SC wanatafuta mchawi na wanatapatapa kwa sababu ya kurundika mizigo pale, Young Africans huo ujinga wameachana nao na ukiwatazama unawaona kabisa wanaelekea wapi, ndio soka la kisasa linataka mipango kama hiyo”
“Unaanzaje kumponda Bigirimana! Kacheza Ulaya EPL sio wa kawaida huyo ana kitu tazama yule beki Mutambala ametajwa kwenye kikosi bora cha (CAF) miaka kadhaa nyuma hao ni baadhi tu”
“Sasa angalia Simba, timu iko pre season bado unafanya ‘Ana Ana Anadoo’ za usajili, lini timu ita concentrate na program za mwalimu?!” amesema Meck Mexime ambaye aliwahi kuvinoa vikosi vya klabu za Mtibwa Sugar na Kagera Sugar