Kocha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Nabi amechimba mkwara kambini AVIC Town, akiwataka wachezaji kupambana mazoezini, ili kujihakikishia nafasi kwenye kikosi chake cha kwanza.

Young Africans ilianza kambi ya maandalizi ya msimu mpya 2022/23, huku ikiwa na wachezaji watano wapya wa Kimataifa, ambao wameanza kuhatarisha nafasi za baadhi ya wachezaji kwenye kikosi cha kwanza.

Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema wachezaji wote wanapaswa kupambana ili kumdhihirishia nani atapaswa kuanza kwenye kikosi cha kwanza msimu ujao.

Amesema msimu ujao ataanza upya, kwani hakuna mchezaji mwenya namba ya kudumu Young Africans, hivyo uwajibikaji wa kila mmoja kwenye mazoezi, utafanikisha kumpa nafasi kwenye kikosi chake cha kwanza.

“Hakuna mchezaji wenye namba ya kudumua Young Africans, ni kama tumeanza upya kwa sasa, kwa yoyote atakayenishawishi katika mazoezi nitampa nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza.”

“Ninaona kila mmoja anajitahidi tangu tulipoanza maandalizi yetu kuelekea msimu ujao, hivyo nina imani nitakua na wachezaji imara na watakaokuwa tayari kupambana wakati wowote msimu ujao.”

“Nafurahi kuona wachezaji wanapambana sana.”

Wachezaji wa kigeni waliosajiliwa Young Africans katika kipindi hiki ni Young Africans imesajili wachezaji watano wa Kimataifa ambao ni Lazarius Kambole (Zambia), Bernard Morrison (Ghana), Gael Bigirimana (Burundi), Joyce Lomalisa (DR Congo) na Stephen Aziz Ki (Burkina Fasso).

Wachezaji walioachwa ni Deus Kaseke, Paul Godfrey ‘Boxer’, Yassin Mustapher (Tanzania) na Chiko Ushindi (DR Congo).

Juma Pondamali: Taifa Stars inakwenda kumaliza
Milioni 91 wakutwa na ugonjwa wa ini