Mwanamuziki nyota kutoka nchini Niger,ia Burna Boy siku baada ya siku amekuwa akiweka rekodi ya kujaza maelfu ya watu katika kumbi zote za ziara yake inayoendelea ya ‘Love, Damini’ na katika onyesho lake la hivi karibuni lililofanyika huko Atlanta, mwimbaji huyo ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Grammy aliujaza Uwanja wa State Farm Arena wenye uwezo wa kuchukua watu 20,000.
Tamasha hilo, lililofanyika Jumapili tarehe 31 Julai 2022 limeingia kwenye rekodi mpya ya nyota huyo, ambaye amekuwa akiisisimua idadi kubwa ya mashabiki kwa uimbaji na uchezaji wake wa kuvutia.
Kufikia sasa, matamasha ya Burna Boy yameonyesha nuru ya kulivutia kundi kubwa la Waafrika walioko ughaibuni, na watu wa rangi zote ambao wanazidi kutekwa na aina muziki wa Afro beats.
Tangu aanze kupata mafanikio ya kupokelewa vizuri kimataifa, Burna Boy ameendelea kujiimarisha zaidi kiasi cha kuingia kwenye orodha ya wasanii, wenye kuutangaza zaidi muziki wa Afrobeats.
Ukubwa wa mwimbaji huyo, hauishii kwenye majukwaa pekee, Burna anaendelea kufanya vizuri hata kwenye digital platforms akiwa na zaidi ya streams bilioni 2, kwenye mtandao wa Spotify.
Mwaka uliopita, alifanikiwa kushinda tuzo za Grammy, miongoni mwa tuzo kubwa ulimwenguni zenye kutamaniwa na kundi kuwa la wasanii.
Alishinda Tuzo tatu mfululizo za BET, na cha kustaajabisha zaidi, amefanikiwa kujaza kumbi za hadhi ya juu duniani kote, ambazozinamuweka kwenye chumba cha peke yake kwenye historia ya wasanii kutoka Afrika, waliowahi kuweka rekodi za kipekee.
Mwaka 2022, pia Burna Boy amefanikiwa kuujaza uwanja maarufu duniani Madison Square Garden, wenye kuchukua watu 20,000 mpaka 20,300 Accor Arena huko Ufaransa, kwa 16,500, Ahoy Arena, na Ziggodome watu 17k huko Holland, Kituo cha Toyota watu 19,000, Houston, na sasa 0001, State Farm Arena huko Atlanta.
Rekodi ambazo amekuwa akiziweka mwanamuziki Burna boy, zinamfanya kuendelea kujidhihirisha kama mmoja wa wasanii wakubwa zaidi, ambao wamewahi kutokea barani Afrik na pengine akawa mwimbaji bora zaidi wa kizazi hiki.