Mkurugenzi wa Ufundi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Saad Kawemba, amesema kikosi chao kipo katika Maandalizi Kabambe ya Mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC.

Miamba hiyo ya Kariakoo itapapatuana Jumamosi (Agosti 13), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku Young Africans akiwa mtetezi wa Ngao hiyo baada ya kuitwaa Msimu uliopita.

Kawemba amesema baada ya Tamasha la Siku ya Mwananchi, Kikosi chao kimerejea kambini kujiandaa na mchezo huo, huku wakiamini wanakwenda kutetea kilicho halali kwao.

“Kwa bahati nzuri tunakwenda kwenye mchezo huu tukiwa watetezi wa Ngao ya Jamii, kwa hiyo tuna kila sababu ya kujiandaa vizuri ili kuona kwamba mashabiki wetu wanapata kile wanachokitarajia.”

“Lengo letu kubwa ni kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu wa Jumamosi, tunawaomba Mashabiki wetu waje Uwanjani kuipa nguvu timu yao, na sisi kama viongozi tunafanya kazi ya kuhakikisha Mataji tuliyoyatwaa msimu uliopita yanabaki kwetu.” amesema Kawemba

Msimu uliopita Young Africans iliifunga Simba SC 1-0, kupitia kwa Mshambuliaji wao kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele, Mchezo ukichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Matumizi sarafu za kidigitali yapendekezwa
Trump akataa kujibu maswali kwa kiapo