Kampuni ya Data Vision International, inakusudia kuanzisha tamasha la michezo litakalowahusisha watu wa rika zote bila kujali jinsia, ikiwa ni sehemu ya utamaduni wake wa kushiriki mazoezi ya pamoja ili kuimarisha afya.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mradi wa DataVision International, Macmillan George hii leo Agosti 14, 2022 wakati akizungumza na vyombo vya Habari juu ya ushiriki wao katika Tamasha la Marathon, lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Timu ya DataVision International Jogging iliyoshiriki Marathon hii leo Agosti 14, 2022 jijini Dar es Salaam.

Amesema, tayari wamekubaliana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutumia Viwanja vyao vilivyopo Kijitonyama na kwamba ushiriki wao katika mbio hizo za leo unatokana na utamaduni waliojiwekea wa kuchangia jamii kupitia mazoezi.

“Sisi DataVision Joggin Family hii ni sehemu ya utamaduni wetu kuhakikisha tunashiriki mazoezi, ukiwa na afya nzuri hata utendaji wako wa kazi unakuwa mzuri, tunawakaribisha wote kushirikiana nasi kwenye mazoezi, si lazima uwe mfanyakazi bali ni kwa watu wote ambao wanajisikia kuungana na sisi,” amesema Macmillan.

Hata hivyo, ameongeza kuwa lengo kubwa la kufanya mazoezi mbali na kujenga afya pia wanakusudia kuisaidia jamii yenye uhitaji maalum na kwamba wanatarajia siku moja wataandaa tamasha kubwa litakalowajumuisha wadau mbalimbali.

DataVision International, ni kampuni inayojihusisha na mambo ya Tafiti na Takwimu kwa mfumo wa tehama, yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam ambapo mbali na mambo mengine pia imekuwa ikijihusisha na masuala mbalimbali ya kijamii kama ilivyo kwa timu ya DataVision Joggin Family isiyo na ubaguzi wa kijinsia na hata rika kimazoezi.

Kenya: IEBC yasema mfumo wa kuhesabu kura haujadukuliwa
Madini Marathon kuanzishwa 2023