Uongozi wa Simba SC umekanusha taarifa za uwepo wa tofauti kati ya Beki wa Kulia Shomari Kapombe na Kocha Mkuu Zoran Maki aliyerithi mikoba ya Kocha kutoka Hispania Franco Pablo Martin.

Simba SC imekanusha taarifa hizo, baada ya kudaiwa kuwa wawili hao walivurugana saa chache kabla ya mchezo dhidi ya Young Africans, na Kocha Zoran kufanya maamuzi ya kumuweka pembeni.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema taarifa zinazosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii na Vijiwe vya Soka, kuhusu wawili hao sio za kweli na zimepangwa kuvuruga mipango ya klabu hiyo.

Amesema Uongozi wa Simba SC unafahamu kuwa Kapombe alipatwa na majeraha na ndio maana hakuweza kuwa sehemu ya kikosi kilichocheza Jumamosi dhidi ya Young Africans iliyoibuka na ushindi wa 2-1.

“Hakuna ukweli wowote juu ya maneno yanayosemwa kwamba Kapombe ameshindwa kucheza, kisa suala la Kocha Zoran, hilo linasemwa tu huko mitaani lakini sisi tunajua ukweli ulipo.”

Kapombe aliumia, alikuwa majeruhi na sasa amerejea na tunatarajia kumuona katika kikosi kuanzia leo tutakapocheza dhidi ya Geita gold FC.” amesema Ahmed Ally.

Hata hivyo Kocha Zoran na Shomari Kapombe jana Jumanne (Agosti 16) walizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano maalum kuhusu mchezo wa leo Jumatano (Agosti 17) dhidi ya Geita Gold FC.

Kocha Zoran alimtumia Beki Israel Patrick Mwenda katika nafasi ya Ulinzi wa Kulia katika mchezo wa Njao ya Jamii dhidi ya Young Africans.

Dejan Georgijevic awatuliza mashabiki Simba SC
Mashine 27 za Young Africans zatua CAF