Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC Ulimboka Mwakingwe amesema Mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Dejan Georgijevic ana uwezo mkubwa kisoka, na ana matarajia makubwa ya kuona akiwashangaza wanaombeza.

Mwakingwe ambaye kwa sasa ni Kocha wa Soka, amesema amemfuatilia Dejan tangu alipowasili nchini na kujiridhishwa ana uwezo wa kupambana, ila amecheza michezo miwili iliyokuwa na ushindani mkubwa na uhitaji wa matokeo mazuri.

Amesema Mashabiki wa Soka la Bongo wamekua na shauku ya haraka kuona Mshambuliaji huyo kutoka nchini Serbia anafanya makubwa, lakini kwake anaendelea kumpa muda na anaamini atafanikiwa.

“Nimeona mikimbio yake na aina yake ya kucheza ni moja ya mastraika wanaopenda kuwekewa pasi kwenye njia na kufunga kama itatokea kuna kiungo wa Simba akamjulia katika hilo atafanya vizuri,”

“Unajua Mashabiki wengi wa Tanzania wamekua na kasumba ya kutaka kuona vitu vikitokea kwa haraka haraka, lakini kwangu mimi sipo hivyo, ninaamini huyu jamaa atawashangaza wengi, hapa kinachomsumbua ni mfumo wa timu lakini akishafahamiana vizuri na viungo, hapo mambo yatamnyookea.” amesema Ulimboka.

Dejan amesajiliwa Simba SC baada ya kupendekezwa na Kocha Mkuu Zorana Maki, huku akichukua nafasi ya Washambuliaji Meddie Kagere na Chriss Mugalu ambao waliachwa kwenye usajili wa klabu hiyo msimu huu 2022/23.

Mudathir Yahya ajiweka pembeni
Dejan Georgijevic awatuliza mashabiki Simba SC