Wajumbe kutoka nchini Marekani wamefika nchini Kenya, Agosti 18 asubuhi, kwa mazungumzo na rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta, rais mteule William Ruto na kiongozi wa Azimio Raila Odinga.

Katika taarifa iliyotolewa na Balozi wa Marekani nchini Kenya, Meg Whitman, wajumbe hao wanataongozwa na Seneta wa Marekani kutoka Delaware.

Balozi wa Marekani nchini Kenya, Meg Whitman akimlaki Seneta wa Marekani kutoka Delaware. Picha: Meg Whitman. Chanzo: Twitter/Tuko

Wajumbe hao pia watafanya mkutano na viongozi wenye ushawishi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali, watoa huduma za afya pamoja na wahifadhi.

“Wajumbe wanaoongozwa na Seneta Chris watakutana na wahifadhi, watoa huduma za afya, na mashirika yanayofanya kazi kuwawezesha wasichana, pia wameratibiwa kukutana na Rais Kenyatta, William Ruto na Raila Odinga ili kujadili malengo ya pamoja, afya, usalama na ustawi wa kiuchumi,” Whitman alisema.

Kuwasili kwa wajumbe hao Marekani kunakujia siku mbili baada ya balozi Whitman kuipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kuendesha uchaguzi wa amani.

Katika taarifa yake, Whitman alibainisha kuwa hatua ya IEBC kumtangaza William Ruto kuwa Rais Mteule ilikuwa muhimu katika mchakato wa uchaguzi.

Ruvu Shooting waitumia salamu Mtibwa Sugar
Mtunisia: Kwa simba hii muda utaongea