Kiungo Mshambuliaji wa Singida Big Stars Deus Kaseke amefunguka kwa mara ya kwanza, baada ya timu hiyo kukusanya alama sita kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Singida Big Stars ilianzia nyumbani Uwanja wa Liti mjini Singida, na kukonga nyoyo za Mashabiki wa mji huo, ambao wamefarijika kuona soka likirejea, baada ya Singida United kushuka Daraja misimu minne iliyopita.

Kaseke amesema timu yao ipo vizuri na imedhidhirisha hilo kwa kuonyesha kandanda safi lililowapa matokeo kwenye michezo iliyopita, hivyo ameendelea kuwasisitiza mashabiki kuwapa ushirikiano.

Amesema wataendelea kupambana ili kufanikisha lengo la timu hiyo, ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu, ikipanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza kwa jina na DTB na kisha kubadilisjwa na kuwa Singida Big Stars

“Singida Big Stars ina wachezaji wengi wazefu na wenye uwezo binafsi, ndiyo maana umefuatilia kwenye michezo yetu miwili iliyopita tulikutana na ushindani mkubwa kwa sababu wapinzani wetu wameshajua tupo vipi.”

“Tutapambana kwenye kila mchezo na kama Kocha alivyosema kila mchezo tutacheza kama fainali na tutafanya hivyo kulingana na mazingira ambayo yapo kwenye timu, tuna wachezaji wazuri na bora sana.”

Singida Big Stars imecheza michezo miwili na kushinda yote ikichapa Tanzania Prisons 1-0, kisha mchezo wa pili ikailaza Mbeya City 2-1.

Binti aliyezama akiogelea alikua 'mboni ya familia'
Nassoro Kapama aigomea Simba SC