Kocha Mkuu wa Simba Queens, Sebastian Nkoma, amesema Kikosi chake kipo tayari kwa Mchezo wa Fainali wa Kuwania nafasi ya Kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mwaka 2022 nchini Morroco, Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’.

Simba Queens ilipata Tiketi ya kucheza Fainali ya Michuano hiyo, kwa kuichapa AS Kigali 5-1 katika mchezo wa Nusu fainali uliounguruma juzi Jumatano (Agosti 24), Uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es salaam.

Simba Queens itacheza dhidi ya She Corporate ya Uganda kesho Jumamosi (Agosti 27), Uwanja wa Azam Complex, endapo itashinda itaweka historia ya kuwa Klabu ya Kwanza Tanzania upande wa Wanawake Kutwaa Ubingwa wa CECAFA na Kukata Tiketi ya Kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Kocha Nkoma amesema amekamilisha Program ya maandalizi ya kuelekea mchezo huo, ambao amekiri utakua mgumu kutokana na kubeba sifa ya FAINALI, lakini akasisitiza kuwa na uhakika wa kupambana na kuchomoza na ushindi.

Amesema Wachezaji wake wameonesha utayari wa kwenda kupambana na wanahimizana kufanya hivyo kila wakati, kutokana na kutambua umuhimu wa mchezo huo.

“Ni mchezo mgumu kwetu, tunahitaji kushinda, tunaendelea kujipanga vizuri. Ninaamini tutashinda na kufikia malengo yetu.”

“Wachezaji wangu wamenihakikishia wapo tayari kupambana ili kuweka Rekodi ya kipekee ya kuwa timu ya kwanza kutwaa Ubingwa wa CECAFA na kutinga kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.”

“Baada ya Mchezo wa Nusu Fainali ambao tulishinda 5-1, Wachezaji wote wamekua wakihimizana kuendelea kuwa kitu kimoja ili kumaliza kazi kwenye mchezo wa Fainali, kwa hatua hiyo binafsi ninafarijika sana, kwa sababu mbali na hamasa yangu kama Kocha, nao wamekua wakimizana kucheza kwa bidii.” amesema Mkoma

Simba Queens itakuana na She Corparates kwa mara ya pili katika Michuano hiyo baada ya kupangwa Kundi B, katika mchezo wa kwanza Uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Wenyeji walichomoza na ushindi wa 2-0.

Michezo mingine ya Kundi B, Simba Queens iliichapa Gerde 6-0 na baadae iliibanjuaYei Joint 4-0.

Zoran Manojlović afunguka sakata la John Bocco
Kocha Simba Queens amkingia kifua Opa Clement